(Sehemu ya Kwanza)
SIRI YA UTAUWA
(Hizi ni notes fupi tuu, ili kupata vizuri somo ni muhimu uwe darasani)
1Tim. 3:16
"Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu."
Siri ya Utauwa ni kile kilichofichika
katika mpango wa Mungu alioutimiza duniani katika kuzaliwa, maisha,
mateso, kifo, ufufuko na kupaa kwa Yesu Kristo; ambacho
watu wa ulimwengu huu hawakijui, lakini ndicho kinachofanya Mkristo
akubali kuishi maisha yanayoonyesha kujitoa kwa undani na kikamilifu
kwa Mungu kupitia Kristo Yesu.
Lugha:
Kigiriki: eusebeia (yoo-seb’-i-ah)
Kiingereza: godliness
KWANINI HUITWA SIRI YA UTAUWA?
a. Ni kwasababu hiaikuwa wazi kwa watu wote pasipo kufunuliwa na Mungu.(Efe. 3:1-6)
KatikaMdo. 9:18, tunaona Paulo
baada ya kupokea neema ya Mungu anatolewa kwenye macho yake magamba. Magamba ni
nini? Magamba ni upofu wa kiroho unaoficha yale Mungu anayotaka uyaone.
- Yesu katika kitabu cha Marko 4:11-12, anasema katika ufalme wa Mungu wapo watu ambao watatazama lakini hawataona, watasikiliza lakini hawatasikia. Watu hawa lazima kwanza wamwamini Mungu ndipo watakapoona wazi yale Mungu anayotaka wafanya. Na imani pia ni karama ya Mungu, haipatikani kwa juhudi za kibinadamu. Katika Yn. 6:44, tunaona kwamba hakuna anayeweza kwenda kwa Yesu asipovutwa na Baba - maana yake hata kumjua Yesu ni karama ya Mungu. Hivyo tunapaswa kuwaombea wale ambao tunawahubiria Injili ili magamba yao yaondoke, na Baba awavute kwa Yesu.
Maswali ya Kujiuliza
-
Kwanini unasema Yesu ni Mungu na unamwabudu?
-
Kwanini unaamini kupitia damu ya Yesu pekee,
unapata msamaha wa dhambi?
MISINGI YA SIRI YA UTAUWA
a.
Kudhihirishwa (kuonekana) kwa Mungu katika mwili
kwa njia ya kuzaliwa, maisha, kifo na ufufuko wa Yesu Kristo. (Yn. 1:1,14; Mwa. 1:2-3)
(Usikose sehemu ya Pili)