SIRI YA UTAUWA NA UTAKATIFU
(Sehemu ya II - Summary)
Mwl. Walter Mrisha
SWALI LA MSINGI
Kwanini, wakati mwingine unapokuta makosa madogo madogo
ya kibinadamu katika Biblia, bado unaiamini?
Jifunze Kuchunguza vitu vya tofauti ambavyo
vinaonekana katika Biblia
Kufasiri Biblia kutoka Lugha Moja kwenda Nyingine
kuliingiza upungufu kidogo wa kimakosa katika kunakili maandishi ya Biblia
Mfano katika 1 Nyakati 21:12 – Daudi aliambiwa achague
njaa itakayotokea miaka 3 lakini katika
2 Sam. 24:13 aliambiwa achague njaa itakayotea miaka 7
Kumbuka Lugha Mbalimbali Zilizotumika katika kufasiri
Biblia Biblia
1.
Lugha za Kwanza za Biblia
a.
Agano la Kale – Kiebrania (Hebrew)
b.
Agano Jipya – Kiyunani (Kigiriki)
2.
Biblia ilifasiriwa kutoka Kigiriki >
Latin/Kirumi > Kiingereza > Kiswahili
3.
Biblia ilikuwa Inaandikwa kwa kutumia wino na
unyoya
4.
Kumbuka Biblia – Neno la Mungu (halijakosewa
– limetoka kwa Mungu) + Mungu akimtumia mwanadamu kuandika (anayeweza kukosea)
-
Biblia inaonyesha Mahusiano ya mwanadamu(mwenye
mapungufu) na Mungu(asiye na mapungufu)
-
Mungu alikuwepo kabla Biblia haijakuwepo
-
Neno la Mungu lilikuwepo kabla Biblia
haijakuwepo
-
Neno la Mungu ni zaidi ya Biblia, lakini lazima
utumie Biblia ili kupima Neno la Mungu. Biblia ni kipimo cha uhakiki wa
Neno la Mungu.
-
Biblia – Neno la Mungu lilioandikwa (Maandiko
Matakatifu)
-
Ukisoma Neno la Mungu, ukaona hauelewi –
usikimbilie kusema limekosewa, bali kuwa mvumilivu kusubiri Mungu akueleweshe.
5.
Kuna aina mbili za usomaji wa Biblia
a.
Kusoma kama Mbegu (mwaka mmoja unasoma
yote) – unaweza endelea na Mwalimu alipofikia, tukasoma wote mpaka mwaka uishe
na kila mwaka turudie mara moja. Nitatoa utaratibu kila wiki ya mpango huo wa
kusoma
b.
Kusoma kama Mkate (Neno la Siku – Roho
Mtakatifu analotaka ulifahamu kwa siku au majira fulani)
NAMNA YA KUSOMA BIBLIA NA
KUELEWA
1. Soma kwa maombi (Roho Mtakatifu)
2. Kutumia references (Rejea)
3. Muulize Mwalimu.
4. Unaweza ukatumia website ya
www.biblehub.com/commentary
NB: Huduma Hii kwa Sasa iko Chini ya Kibali na Uongozi wa
Kanisa Takatifu la Mungu (Tegeta-Dar es Salaam), chini ya Mch. Obed Joseph
Katunzi.
MAWASILIANO
------------
MAFUNDISHO - MAOMBI - MAOMBEZI - USHAURI - USHUHUDA
+255 714 766 148 / +255 620 576 148 - Mwl. Walter Moses
Mrisha
Whatsapp Group:
https://chat.whatsapp.com/GXSHLDPN0E1DGEE1nxNKIe
GoogleMeet: meet.google.com/ztj-eetx-teq
Website: www.wanafunziwayesuonline.blogspot.com
Facebook/Youtube: Wanafunzi wa Yesu
E-mail: waltermosesmrisha@gmail.com
VIFAA VYA KUJA NAVYO DARASANI
-----------------------------
* Moyo Ulio Tayari Kujifunza
* Biblia (SUV & KJV)
* Notebook
* Bible Audio