Habari wapendwa rafiki zangu,
Nawasalimu kwa amani, upendo wa dhati na moto wa shukrani unaotoka moyoni mwangu!
Shukrani, heshima na utukufu vyote namrudishia Mungu aliye Hai, aliyeniumba kwa makusudi ya milele ambayo mimi mwenyewe siwezi kuyafahamu kikamilifu.
Nimezaliwa na kukulia Tanzania, nchi yenye baraka na urithi wa kipekee. Mimi ni mtumishi wa Mungu ninayeongozwa na Roho Mtakatifu, mwalimu na mhubiri wa Injili ya Yesu Kristo. Nimejitoa kwa moyo wangu wote kusambaza Habari Njema kwa kila nafsi ambayo Mungu ameniongoza kukutana nayo—kupitia elimu, teknolojia, na mafundisho ya Biblia.
Katika safari yangu kielimu, nimesoma na kuhitimu elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Mwandege (Mwandege Boys Secondary School mwaka 2011. Nilijiunga na masomo ya shahada ya Computer Engeneering, lakini sikukamilisha kutokana na changamoto binafsi nilizopitia wakati huo.
Hata hivyo, baada ya kuokoka mwaka 2018, kwa neema ya Mungu nilipewa nafasi ya kusoma katika Chuo cha Mafunzo na Uongozi Usangi, ambako nilisoma kwa miaka mitatu na kuhitimu kwa kupata Cheti cha Evangelism and Parish Work.
Kwa neema ya Mungu, nimesafiri sehemu mbalimbali za Tanzania nikihubiri na kushuhudia Injili. Leo hii, Mungu amenisimamisha kama mwalimu wa Masomo ya Kompyuta na Lugha (Kiswahili na Kiingereza) katika chuo kilekile nilichosoma. Wanafunzi ninaowafundisha wanatoka pande zote—wa kiinjilisti na wasiokuwa wa kiinjilisti—lakini wote wanaguswa na neema ya Kristo. Wakati huohuo, ninaendelea kufundisha na kuhubiri Neno la Mungu, si tu ana kwa ana, bali pia kupitia njia za mtandaoni, nikifikia nafsi nyingi kwa ajili ya Ufalme wa Mungu.
Ninakuambia, rafiki yangu, kwamba kama mimi, kila mmoja wetu ameumbwa na Mungu kwa makusudi ya milele. Safari yako, elimu yako, talanta zako na kazo, vyote vinaweza kuwa vyombo vya kushughulikia nafsi nyingi na kusambaza mwanga wa Kristo duniani.
Usisubiri mpaka nafasi itakupata, bali chukua hatua leo: jifunze, fundisha, hubiri na tumia kipaji chako kwa ajili ya Ufalme wa Mungu. Kwa neema yake, unaweza kuwa chombo cha mabadiliko katika jamii yako, kueneza upendo, rehema na nuru ya Injili kwa kila mtu unaekutana naye.
Tunaweza pamoja, kwa Kristo, kuathiri dunia kwa maneno, vitendo, na teknolojia. Naomba neema na baraka zake ziendelee kuwa nanyi nyote—wasomaji, wanafunzi, walimu, na kila rafiki anayesoma blogu hii.
Walter Moses Mrisha
Wasilina nami kupitia:
Facebook
Whatsapp: +255 714 766 148
Email: waltermosesmrisha@gmail.com