Mtumishi
wa Mungu Walter Mrisha alipokea wito wa kumtumikia Mungu kipindi
alipookoka tuu, mnamo mwaka 2018. Baada ya kubatizwa, alianza
kuhubiri Injili mitaani na kuombea wagonjwa. Hii ilikuwa katika
mkoa wa Dar es salaam. Baada ya kufanya huduma hiyo miezi kadhaa,
alisafiri kuelekea mkoani Kilimanjaro ili kwenda kujijenga vizuri
kiroho.
Januari 2019, alianza mafunzo ya huduma ya Mungu katika Chuo cha Mafunzo na Uongozi Usangi, kilichopo huko Mwanga-Kilimanjaro na kuhitimu mwaka 2021.
Baada ya kuhitimu, alianza kufanya huduma ya mikutano ya Injili, semina makanisani, uinjilisti wa mtaani na nyumba kwa nyumba, maombi na maombezi katika maeneo mbalimbali ya Tanzania ikiwemo Dar-es-salaam, Tabora, Dodoma, Singida, Arusha, Tanga na Kilimanjaro.
Kwasasa, anamtumikia Mungu kupitia huduma ya Wanafunzi wa Yesu, ambayo iko chini ya kanisa la Revelation and Testimony Church of God (Kanisa Takatifu la Mungu), lenye makao yake makuu Tegeta, Dar-es-salaam.