Tuesday, May 26, 2026

SIRI YA UTAUWA NA UTAKATIFU (Sehemu ya II - Summary)

 

SIRI YA UTAUWA NA UTAKATIFU

(Sehemu ya II - Summary)

Mwl. Walter Mrisha

 

SWALI LA MSINGI

Kwanini, wakati mwingine unapokuta makosa madogo madogo ya kibinadamu katika Biblia, bado unaiamini?

 

Jifunze Kuchunguza vitu vya tofauti ambavyo vinaonekana katika Biblia

Kufasiri Biblia kutoka Lugha Moja kwenda Nyingine kuliingiza upungufu kidogo wa kimakosa katika kunakili maandishi ya Biblia

Mfano katika 1 Nyakati 21:12 – Daudi aliambiwa achague njaa itakayotokea miaka 3 lakini katika  2 Sam. 24:13 aliambiwa achague njaa itakayotea miaka 7

Kumbuka Lugha Mbalimbali Zilizotumika katika kufasiri Biblia Biblia

1.     Lugha za Kwanza za Biblia

a.      Agano la Kale – Kiebrania (Hebrew)

b.     Agano Jipya – Kiyunani (Kigiriki)

2.     Biblia ilifasiriwa kutoka Kigiriki > Latin/Kirumi > Kiingereza > Kiswahili

3.     Biblia ilikuwa Inaandikwa kwa kutumia wino na unyoya

4.     Kumbuka Biblia – Neno la Mungu (halijakosewa – limetoka kwa Mungu) + Mungu akimtumia mwanadamu kuandika (anayeweza kukosea)

-        Biblia inaonyesha Mahusiano ya mwanadamu(mwenye mapungufu) na Mungu(asiye na mapungufu)

-        Mungu alikuwepo kabla Biblia haijakuwepo

-        Neno la Mungu lilikuwepo kabla Biblia haijakuwepo

-        Neno la Mungu ni zaidi ya Biblia, lakini lazima utumie Biblia ili kupima Neno la Mungu. Biblia ni kipimo cha uhakiki wa Neno la Mungu.

-        Biblia – Neno la Mungu lilioandikwa (Maandiko Matakatifu)

-        Ukisoma Neno la Mungu, ukaona hauelewi – usikimbilie kusema limekosewa, bali kuwa mvumilivu kusubiri Mungu akueleweshe.

5.     Kuna aina mbili za usomaji wa Biblia

a.     Kusoma kama Mbegu (mwaka mmoja unasoma yote) – unaweza endelea na Mwalimu alipofikia, tukasoma wote mpaka mwaka uishe na kila mwaka turudie mara moja. Nitatoa utaratibu kila wiki ya mpango huo wa kusoma

b.     Kusoma kama Mkate (Neno la Siku – Roho Mtakatifu analotaka ulifahamu kwa siku au majira fulani)

 

NAMNA YA KUSOMA BIBLIA NA KUELEWA

1.     Soma kwa maombi (Roho Mtakatifu)

2.     Kutumia references (Rejea)

3.     Muulize Mwalimu.

4.     Unaweza ukatumia website ya www.biblehub.com/commentary

 

 

 

NB: Huduma Hii kwa Sasa iko Chini ya Kibali na Uongozi wa Kanisa Takatifu la Mungu (Tegeta-Dar es Salaam), chini ya Mch. Obed Joseph Katunzi.

 

MAWASILIANO

------------

MAFUNDISHO - MAOMBI - MAOMBEZI - USHAURI - USHUHUDA

+255 714 766 148 / +255 620 576 148 - Mwl. Walter Moses Mrisha

 

Whatsapp Group: https://chat.whatsapp.com/GXSHLDPN0E1DGEE1nxNKIe

GoogleMeet: meet.google.com/ztj-eetx-teq

 

Website: www.wanafunziwayesuonline.blogspot.com

Facebook/Youtube: Wanafunzi wa Yesu

E-mail: waltermosesmrisha@gmail.com

 

 

VIFAA VYA KUJA NAVYO DARASANI

-----------------------------

* Moyo Ulio Tayari Kujifunza

* Biblia (SUV & KJV)

* Notebook

* Bible Audio

Siri ya Utauwa na Utakatifu

Siri ya Utauwa na Utakatifu

(Sehemu ya Kwanza)

SIRI YA UTAUWA

(Hizi ni notes fupi tuu, ili kupata vizuri somo ni muhimu uwe darasani)

1Tim. 3:16

"Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu."

Siri ya Utauwa ni kile kilichofichika katika mpango wa Mungu alioutimiza duniani katika kuzaliwa, maisha, mateso, kifo, ufufuko na kupaa kwa Yesu Kristo; ambacho watu wa ulimwengu huu hawakijui, lakini ndicho kinachofanya Mkristo akubali kuishi maisha yanayoonyesha kujitoa kwa undani na kikamilifu kwa Mungu kupitia Kristo Yesu.

Lugha:

Kigiriki: eusebeia (yoo-seb’-i-ah)

Kiingereza: godliness

KWANINI HUITWA SIRI YA UTAUWA?

a.     Ni kwasababu hiaikuwa wazi kwa watu wote pasipo kufunuliwa na Mungu.(Efe. 3:1-6)

KatikaMdo. 9:18, tunaona Paulo baada ya kupokea neema ya Mungu anatolewa kwenye macho yake magamba. Magamba ni nini? Magamba ni upofu wa kiroho unaoficha yale Mungu anayotaka uyaone.

-        Yesu katika kitabu cha Marko 4:11-12, anasema katika ufalme wa Mungu wapo watu ambao watatazama lakini hawataona, watasikiliza lakini hawatasikia. Watu hawa lazima kwanza wamwamini Mungu ndipo watakapoona wazi yale Mungu anayotaka wafanya. Na imani pia ni karama ya Mungu, haipatikani kwa juhudi za kibinadamu. Katika Yn. 6:44, tunaona kwamba hakuna anayeweza kwenda kwa Yesu asipovutwa na Baba - maana yake hata kumjua Yesu ni karama ya Mungu. Hivyo tunapaswa kuwaombea wale ambao tunawahubiria Injili ili magamba yao yaondoke, na Baba awavute kwa Yesu.

Maswali ya Kujiuliza

-        Kwanini unasema Yesu ni Mungu na unamwabudu?

-        Kwanini unaamini kupitia damu ya Yesu pekee, unapata msamaha wa dhambi?

MISINGI YA SIRI YA UTAUWA

a.      Kudhihirishwa (kuonekana) kwa Mungu katika mwili kwa njia ya kuzaliwa, maisha, kifo na ufufuko wa Yesu Kristo. (Yn. 1:1,14; Mwa. 1:2-3)

(Usikose sehemu ya Pili)

SIRI YA UTAUWA NA UTAKATIFU (Sehemu ya II - Summary)

  SIRI YA UTAUWA NA UTAKATIFU (Sehemu ya II - Summary) Mwl. Walter Mrisha   SWALI LA MSINGI Kwanini, wakati mwingine unapokuta mak...