Sunday, September 28, 2025

MADHARA YA KUBAKI UKIKAA KATIKA MAZINGIRA YA KIROHO AMBAYO MUNGU AMEKWAMBIA USIKAE


Mwl. Walter M. Mrisha 

1. MALENGO YA SOMO

1.1. Kujua njia au mazingira ambayo shetani ameyatengeneza ili ushindwe kufanya au kufikia malengo ya Mungu katika safari yako hapa duniani ya kwenda mbinguni.

1.2. Kufahamu mipango ya Mungu anayoitumia ili kuilinda nafsi yako kusudi iweze kupokea baraka alizokusudia uzipokee katika Ufalme wake hapa duniani na mbinguni.

2. UTANGULIZI

2.1. Msingi wa somo: Hes. 33:50-56; Yos. 23:12-13

2.2. Maana ya neno mazingira ya kiroho

Kwa kadiri neno hili litakavyotumika katika somo, mazingira ya kiroho ni hali ya kiroho iliyoko katika eneo fulani inayosababishwa na aina ya maisha ya kiroho wanayoishi watu wa eneo hilo.

Mfano wa mazingira ya kiroho: mahusiano, tabia, tamaduni, kampuni, taasisi, biashara, dini, mtandao, ardhi, ulimwengu huu n.k

2.3. Ili Mungu akufanikishe katika eneo alilokusudia kukuweka, lazima uhakikishe unashirikiana naye katika kutengeneza mazingira mazuri ya kiroho ukiwa kakatika eneo hilo; kusudi mazingira yasikukwamishe kupokea baraka zake.

3. MADHARA YA KUBAKI UKIKAA KATIKA MAZINGIRA YA KIROHO AMBAYO MUNGU AMEKWAMBIA USIKAE

3.1. Kumzuia Mungu asitekeleze kwa ufanisi mipango na malengo yake mema aliyonayo juu ya maisha yako.

3.2. Kushindwa kustahimili nguvu za upinzani wa shetani zilizoko katika mazingira hayo kutokana na upungufu wa nguvu za kiroho ndani yako (1Kor. 10:13; Mdo. 1:4, 8)

3.3. Kumpa shetani nafasi ya kutumia mazingira hayo kuwa sindano, mwiba, mjeledi, tanzi na mtego kwako kwa njia zifuatazo:

i. Kukufanya usione vizuri au bayana jinsi Mungu anavyotaka uone au uenende sawasawa na mapenzi yake kwako. (sindano machoni)

ii. Kukufanya usifanye maamuzi sahihi kwenye maisha mbali na kile kitu ambacho Mungu amechagua ukifanye (sindano machoni)

iii. Kukupa maumivu ya muda mrefu, yatakayokukera (kukusumbua) na kukukosesha raha katika maisha yako. (mwiba/mjeledi)

iv. Kukufunga kiroho, kimwili au kiakili kisha kuua vile ambavyo Mungu alitaka uishi hapa duniani na mbinguni (tanzi/mtego)

3.4. Kushawishika kuabudu kinyume na namna Mungu alivyoagiza uabudu (Zab. 103:34-38)

3.5. Humzuia Mungu asiweze kukukwepesha adhabu aliyokusudia kwa watu waliokuwa wanakaa katika mazingira ya namna hiyo (Hes. 33:55-56; Mwa. 19:12-26)

3.6. Kumzuia Mungu asiweze kuendelea kufukuza adui zake walioko mbele zako wanaoweza kukukwamisha usifikie malengo yake aliyoyaweka kwako (Yos. 23:13a;Kumb. 9:3-4; Yak. 4:4)

4. MAZINGIRA YANAYOWEZA KUWA MWIBA, MJELEDI, SINDANO, TANZI AU MTEGO KWAKO

4.1. Kuruhu nafsi yako kurudi nyuma kiimani (Yos. 23:12a)

Mfano kupoa katika kusoma Neno, kuomba, kushiriki ibada, kushuhudia n.k.

Hufungua mlango wa shetani kupata uhalali kulipiza kisasi baada ya wewe kumkimbia tangu ulipomwamini Mungu.

4.2. Kufungwa nira pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawasawa (2Kor. 6:14-18)

Wasioamini ni watu wote ambao hawajui au hawakubali au wanafanya vita juu ya ukweli, kwa sehemu au kwa yote, wa yale yaliyofunuliwa na Mungu katika Maandiko Matakatifu (Biblia).

A. Namna unavyoweza kufungwa nira kwa jinsi isivyo sawasawa na wasioamini:

i. Kukubali kufuata sheria au taratibu zisizo na imani katika ufunuo kamili wa Mungu katika Neno lake (Mdo.15:10-11; Gal. 3:10; 5:1).

a) Nira ya dini: ibada za sanamu (Kut. 20:4-5); ibada za kuwaombea wafu (Ebr. 9:27, Lk. 16:19-31; 2 Kor. 5:10; Lk. 23:43) ibada za jua, mwezi au nyota ( Kumb. 4:19) sikukuu za kidini zisizo na msingi katika Neno (Kumb. 12:29-30; Mk. 7:7; Lk. 2:13-14).

b) Nira ya dhehebu: ubatizo wa wasio na imani ya wokovu, mfumo sadaka zisizo na msingi katika Neno,

c) Ofisi/biashara/kazi: kulazimika kufanya kazi za kipato siku ya sabato

d) Mila na tamaduni: matambiko

e) Mitindo ya dunia: muziki, mavazi, lugha za kidunia

ii. Kuwa na mahusiano ya karibu sana na mtu asiyemwabudu Mungu katika agano ulilonalo na Mungu kupitia Yesu Kristo (kv. Ndoa, urafiki wa karibu n.k)(Yos. 23:12-13; Kumb. 7:2-4)

B. Kufungwa nira kwa jinsi ilivyo sawasawa na wasioamini

a) kuhakikisha kila unachoshirikiana na wasio amini hakiondoi utumishi wako kwa Yesu (Mt. 11:29-30)

b) Kuhakikisha mwenendo wako mbele ya uliofungwa nira nao hauharibu heshima ya jina la Mungu na Neno la Mungu (1 Tim. 6:1)

 

5. MAMBO YA KUFANYA ILI UWEZE KUTENGENEZA MAZINGIRA YA KIROHO KATIKA ENEO

5.1. Mwite Mungu kwa kupitia maombi ili awe juu ya hilo eneo, ajitukuze kwa kutekeleza hukumu na utakaso juu yake (Eze. 28:20-24)

a) Mungu ajulikane na aonekane yuko juu zaidi ya hayo mazingira

b) Mungu ahukumu roho za adui zilizopo katika eneo

c) Mungu atakeleze utakaso kwako na katika eneo (kupitia utakaso, Mungu atakutenga na mazingira hayo)

Ubatizo Sahihi ni Huu

Ubatizo Kibiblia Utangulizi Moja ya somo Muhimu sana kwa mkristo anayetarajia...